TOGO-SIASA-USALAMA

Mazungumzo baina ya wanasiasa kuanza Togo

Mwezeshaji wa mazungumzo, Nana Akufo-Addo, Rais wa Ghana, aliwasili siku ya Jumapili mchana katika mji mkuu wa Togo.
Mwezeshaji wa mazungumzo, Nana Akufo-Addo, Rais wa Ghana, aliwasili siku ya Jumapili mchana katika mji mkuu wa Togo. REUTERS/Luc Gnago

Kamati ya maandalizi ilikamilisha kazi yake siku ya Jumapili, Februari 18, baada ya majadiliano marefu. Hati ya mazungumzo hayo ilitangazawa na itatumika kwa kuendeleza mazungumzo ya kisiasa ambayo yatakua yakiendelea.

Matangazo ya kibiashara

Ni hati ya ukurasa nne ambayo itatumika kama sheria ya ndani wakati wa mazungumzo kati ya wanasiasa wa kutoka chama tawala na washirika wake na upinzani. Wajumbe saba kutoka kila upande wamealikwa kwenye meza ya mazungumzo chini ya uenyekiti wa Mwezeshaji, ambaye ni Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo.

Mazungumzo yatadumu siku kumi. Mazungumzo hayo yana malengo matatu: kufikia makubaliano kuhusu masuala maalum yanayotokana na mgogoro wa sasa, kukubaliana juu ya hatua thabiti za kurejesha imani kati ya wanasiasa wa mgogoro huo na kuanzishwa kwa mfumo wa utekelezaji wa makubaliano kutoka mazungumzo hayo na ufuatiliaji wake.

Katika ajenda ya mazungumzo hayo, mambo kumi na mbili yameorodheshwa kwa makubaliano ya pamoja ikiwa ni pamoja na kujelea upya Katiba ya mwaka 1992, kuandaa kura ya maoni juu ya marekebisho ya Katiba.