DRC-VIRUNGA-RWANDA-WANAHABARI

Wanahabari wazuiwa kufika katika eneo la vita kati ya jeshi la DRC na Rwanda

Wanahabari wa DRC wakiwa katika mbuga ya wanyama ya Virunga
Wanahabari wa DRC wakiwa katika mbuga ya wanyama ya Virunga Chube Ngrombi/Correspodent RFI Goma

Wanahabari zaidi ya 10 wa DRC na wa Kimataifa pamoja na viongozi wa jeshi la DRC Katika jimbo la Kivu Kaskazini, wamezuiwa kufika katika mbuga ya wanyama ya Virunga.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya kutembea kwa miguu na kutumia usafiri wa gari, wanahabari hao wakiwa na wanajeshi walikuwa na lengo la kufika katika eneo la Visoke, kulikoshuhudiwa mapigano kati ya wanajeshi wa DRC na Rwanda.

Jeshi la DRC, linasema kuwa wanajeshi wake sita walipoteza maisha katika makabiliano hayo.

Kamanda wa jeshi katika Jimbo la Kivu Kaskazini Jenerali Bruno Mandefu amesema, hatua ya kutowaruhusu wabahabari hao imekuja kwa sababu wachunguzi wa Jumuiya ya ukanda wa Maziwa Makuu hawakutana kufanya uchunguzi huo na wanahabari.

"Sisi tulikuwa tumezani kwamba ni Rwanda ndiyo ya sababisha kurejea nyumbani pasipo kufikia lengo letu ,tumefurahi kupata mwangaza,tume choshwa lakini tunaipenda nchi yetu,tuna subiri uchunguzi wa CIRGL" alisema Mwanahabari mmoja.