DRC, UDPS-CENI-SIASA

Chama cha UDPS hakina imani na tume ya Uchaguzi DRC

Makao makuu ya chama cha UDPS Kinshasa.
Makao makuu ya chama cha UDPS Kinshasa. RFI/Sonia Rolley

Chama kikuu cha upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo UDPS kimesema kuwa hakina imani na tume ya uchaguzi nchini humo CENI katika kuandaa uchaguzi mkuu ulio huru na haki.

Matangazo ya kibiashara

Kauli ya upinzani inatolewa wakati huu ambapo juma moja lililopita mkuu wa CENI Corneil Nangaa alisema huenda uchaguzi mkuu usifanyike mwishoni mwa mwaka huu kama ulivyopangwa ikiwa time yake haitapata mitambo ya kielektroniki ya kutambua wapiga kura.

Naibu katibu mkuu wa UDPS Reubens Mikindo akiongea na idhaa ya Kiswahili ya RFI amesema kuna njama za kuhakikisha uchaguzi mkuu haufanyiki mwishoni mwa mwaka huu.

Katika hatua nyingine rais Joseph Kabila amemteua katibu mkuu wa chama tawala PPRD, Henri Mova Sakanyi kuwa waziri mpya wa mambo ya ndani na naibu waziri mkuu.