AFRIKA KUSINI-USALAMA

Polisi 5 na askari 1 wauawa na watu wenye silaha Afrika Kusini

Mji wa Cap, Afrika kusini, ambapo polisi watano na askari mmoja waliuawa na kundi la watu wenye silaha..
Mji wa Cap, Afrika kusini, ambapo polisi watano na askari mmoja waliuawa na kundi la watu wenye silaha.. CC/Pixabay/sharonang

Polisi watano na askari mmoja wameuawa na kundi la watu wenye katika mashambulizi dhidi ya kituo cha polisi katika mji mdogo kusini mashariki mwa Afrika Kusini leo Jumatano.

Matangazo ya kibiashara

Kundi la watu wenye silaha walifanya mashambulizi dhidi ya kituo cha polisi cha Engcobo katika mkoa wa Cape mashariki baada ya usiku wa manane leo Jumatano.

Kundi hili liliwafyatulia risase polisi na kuwashikilia mateka wawili miongoni mwao.

"Mapema leo asubuhi, watu sita waliuawa wakati genge la wezi walifanya mashambulizi dhidi ya kituo cha polisi," msemaji wa polisi Vish Naidoo ameliambia shirika la habari la AFP.

"Watu watano kati ya sita waliouawa walikuwa polisi, watatu walipigwa risasi katika kituo cha polisi wakati wezi walipofyatua risasi kiholelea," msemaji wa polisi ameongeza.

Washambuliaji walichukua maofisa wengine wawili wa polisi na kuwaingiza katika gari, ambapo miili yao ilipatikana baadaye upande wa barabara. Pia waliua askari mmoja.

Polisi hawakuweza kufafanua mara moja sababu za za shambulio hilo baya.

Mashambulizi dhidi ya polisi yanafanyika mara kwa mara nchini Afrika Kusini, ambayo inavunja rekodi kwa viwango vya juu zaidi vya uhalifu duniani.

Maafisa wa polisi wasiopungua 57 waliuawa wakiwa kazini kati ya mwezi Aprili 2016 na mwezi Machi 2017, kulingana na takwimu rasmi rasmi.