Baadhi ya wanafunzi waliotekwa na Boko Haram wapatikana

Kundi la wasichana 82 wanafunzi wa Chibok waliachiliwa na Boko Haram Mei 6, 2017.
Kundi la wasichana 82 wanafunzi wa Chibok waliachiliwa na Boko Haram Mei 6, 2017. REUTERS/Zanah Mustapha

Jeshi la Nigeria limetangaza kwamba limefaulu kuwarejesha kutoka mikononi mwa Boko Haram wanafunzi waliokua wametekwa na kundi hilo. Jeshi linaendelea kutafuta wanafunzi wengine ambao bado wako mikononi mwa kundi hili hatari.

Matangazo ya kibiashara

Wasichana 76 na miili ya wasichana wengine wawili ambao walitoweka baada ya shambulio lililondeshwa na wapiganaji wa Boko Haram katika kijiji kimoja kaskazini mashariki mwa jimbo la Yobe kaskazini mashariki mwa Nigeria, wazazi wa wasichana hao na afisa mmoja wa serikali wameliambia shirika la habari la Reuters.

Lakini kwa mujibu wa shirika la habari la AFP likimnukuu Gavana wa jimbo la Yobe, Abdullahi Bego, limesema kuwa wanafunzi waliopatikan ani 111.

Wanafunzi zaidi ya 100 walitoweka baada ya shambulio hilo katika kijiji cha Dapchi, ikiwa ni kisa cha utekaji nyara cha aina yake tangu kutekwa nyara kwa wanafunzi 270 mnamo mwaka 2014 kutoka shule ya Chibok.

Rais Muhammadu Buhari amewaagiza mawaziri wake wa ulinzi na wa mambo ya nje kwenda kaskazini-mashariki mwa nchi Nigeria kupata taarifa zaidi kuhusu hali hiyo, Waziri wa Habari wa Nigeria, Lai Mohammed, ameliambia shirika la habari la Reuters.

Mpaka sasa wanafunzi wengine bado hawajapatikana na haijulikani kama waliuawa au bado wako hai.