ISRAEL-AFRIKA-WAHAMIAJI-USALAMA

Wahamiaji kutoka Afrika wazuiliwa Israel

Nje ya kituo cha Holot, katika jangwa la Negev, mamia ya wahamiaji haramu wa Kiafrika walioachiliwa na Israeli wanajiandaa kuchukua basi (picha yazamani).
Nje ya kituo cha Holot, katika jangwa la Negev, mamia ya wahamiaji haramu wa Kiafrika walioachiliwa na Israeli wanajiandaa kuchukua basi (picha yazamani). Murielle Paradon / RFI

Mamlaka ya Israeli inaendelea kutekeleza mpango wake wa kuwafukuza nchini humo wahamiaji 40,000, hasa kutoka nchini Eritrea na Sudan.

Matangazo ya kibiashara

Mpango wa serikali unawapa watu wanaolengwa na hatua hiyo kuchagua kati ya kuondoka nchini Israel kwa "hiari" na kwenda nchi nyingine au kuzuiliwa jela kwa muda usiojulikana. Siku ya Jumanne, Februari 20, kwa mara ya kwanza, wahamiaji saba waliokataa kuondoka nchini Israeli walifungwa.

Wahamiaji saba waliofungwa siku ya Jumanne walikuwa miongoni mwa watu 750 wanaozuiliwa wakati huu katika kituo cha Holot. Kituo hiki ambacho ni kama nusu jela kilifunguliwa katika jangwa la Negev, ili kuwaweka pamojaraia hao wa kigeni walioingia nchini Israeli kinyume cha sheria. Na serikali sasa inataka kufunga kituo hicho.

Raia hawa saba wa Eritrea walipokea wito kutoka kwa mamlaka ya Israeli mwezi Januari. Walipewa mwezi mmoja ili kuamua kati ya kuondoka "kwa hiari" na kwenda nchi nyingine au kuzuiliwa kwa muda usiojulikana. siku ya Jumanne, watu hawa saba waliitwa na idara ya uhamiaji katika kituo cha Holot. Kwa mujibu wa mmoja wa wafungwa hao aliyehojiwa na RFI, walitakiwa kutoa jibu lao. Raia hawa saba wa Eritrea walichagua kufungwa badala ya kuondoka nchini Israeli.

Mamlaka ya Israeli iliwahamishia katika gereza la Saharonim, zaidi ya kilomta mia moja kutoka Holot. Lakini wahamiaji hawa hawakuweza kuweka sawa nguo zao na vitu vingine. Hatua hii ya haraka inaonekana kama ukatili na wafungwa wa Holot. Kama ishara ya maandamano, wote waliamua kuanza mgomo wa kususia chakula tangu Jumanne usiku.