RWANDA-DRC-WAKIMBIZI-USALAMA

Wakimbizi 5 wa DRC wauawa katika maandamano Rwanda

Wakimbizi wa DRC wanapewa hifadhi katika kambi ya Kiziba, mashariki mwa Rwanda.
Wakimbizi wa DRC wanapewa hifadhi katika kambi ya Kiziba, mashariki mwa Rwanda. DR

Polisi nchini Rwanda imetangaza leo Ijumaa kwamba wakimbizi wasiopungua watano kutoka DRC ndio waliuawa katika maandamano dhidi ya uamuzi wa kupunguziwa mlo katika kambi yao ya Kiziba, mashariki mwa Rwanda.

Matangazo ya kibiashara

Katika vurugu hizo wkimbizi 20 walijeruhiwa kwa mujibu wa polisi ya Rwanda.

Hata hivyo polisi ya Rwanda inadai kuwa katika ghasia hizo polisi saba walijeruhiwa.

Takriban wakimbizi 3,000 kutoka DRC wanaendelea kuandamana tangu siku ya Jumanne nje ya ofisi ya Umoja wa Mataifa dhidi ya uamuzi wa Shirika la la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) wa kupunguza mlo katika kambi yao.

Siku ya Alhamisi Polisi ilijaribu kutawanya umati wa wakimbizi kwa kutumia mabomu ya machozi , msemaji wa polisi amesema.

"Tulitumia nguvu jana mchana, baada ya kutoa onyo kwamba vikosi vya usalama vitaingilia kati," amesema Theos Badege kwenye redio ya serikali.

"Walianza kutupa mawe, vipande vya chuma, na kwa yote hayo, wakimbizi 20 walijeruhiwa, pamoja na maafisa wa polisi saba," ameeleza kwa kina. "Wakimbizi watano walipoteza maisha."

Kupitia akaunti yake ya Twitter, polisi ya Rwanda pia imetangaza kwamba inawashikilia wakimbizi 15.

Wakimbizi waliondoka katika kambi yao ya Kiziba, kilomita 15 kutoka mji wa Karongi, magharibi mwa Rwanda, ili kupinga uamuzi wa UNHC wa kuwapunguzia mlo kwa 25%. Uamuzi ambao ulianza kutekelezwa mwezi uliopita na UNHCR. Wakimbizi 17,000 kutoka DRC ndio wanapewa hifadhi katika kambi hii.

Rwanda inawapa hifadhi wakimbizi 174,000 kwa jumla, ikiwa ni pamoja na 57,000 kutoka Burundi waliokimbia ghasia za nchi mwaka 2015. Wengine ni kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), nchi inayokabiliwa mara kwa mara na ukosefu wa usalama tangu miaka 20 sasa.