SOMALIA-USALAMA-MOGADISHU

Watu 18 wauawa baada ya shambulizi la kigaidi mjini Mogadishu

Shambulizi la kigaidi la Al Shabab mjini Mogadishu  nchini Somalia
Shambulizi la kigaidi la Al Shabab mjini Mogadishu nchini Somalia REUTERS/Feisal Omar

Watu 18 wameuawa na wengine 20 kujeruhiwa mjini Mogadishu nchini Somalia, baada ya milipuko miwili ya bomu iliyokuwa imetegwa ndani ya gari ndogo.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti za polisi zinasema kuwa shambulizi hilo lililenga Ikulu ya rais na hoteli ya kifahari.

Kundi la kigaidi la Al Shabab limedai kutekeleza shambulizi hili na kusema lilikuwa linawalenga maafisa wa serikali.

Magaidi wa Al Shabab kwa muda mrefu wamekuwa wakipigana kuipindua serikali ya Somalia inayotambuliwa Kimataifa.

Mwezi Oktoba mwaka 2017, ilitekeleza shambulizi baya zaidi mjini Mogadishu na kusababisha vifo vya watu 500.

Umoja wa Afrika umetuma wanajeshi 22, 000 tangu mwaka 2007 kwa lengo la kupambana na magaidi hao lakini pia kuilinda serikali ya Mogadishu.

Al Shabab ni kundi linalosalia hatari kwa usalama wa ukanda wa Afrika Mashariki.