DRC-USALAMA

Mji wa Goma wakabiliwa na ukosefu wa usalama

Askari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakiwasaka waasi wanaohatarisha usalama katika mji wa Goma.
Askari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakiwasaka waasi wanaohatarisha usalama katika mji wa Goma. REUTERS/Kenny Katombe

Hali ya wasiwasi imeendelea kushuhudiwa jijini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya waasi 4 kuuawa na wengine 7 kukamatwa katika mapigano yaliyotokea katika mji huo kati ya waasi wa Mai Mai na jeshi la DRC (FARDC) mwishoni mwa wiki iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Guillaume Djike msemaji wa jeshi la FARDC katika operesheni za kivita sokola ya pili katika mkoa wa Kivu Kaskazini ameiambia Idhaa ya Kiswahili ya RFI kwamba, katika juhudi za kutafuta usalama jijini Goma, jeshi la Congo (FARDC) lillipopata taarifa mwishoni mwa wiki iliyo pita kwamba kuna waasi ambao walijijaribu kushambulia mji wa Goma, FARDC ilifanya kazi yake kwa kuwashambulia waasi hao jambo ambalo hadi sasa limepelekea raia kuishi kwa wasiwasi katika mji huo.

“Tunaendelea kufwatilia wahalifu hao wa Mai Mai, kati yao wa nne wameuawa, tisa wamejeruhiwa,saba wameekamatwa na upande wa jeshi la Congo tumempoteza askari wetu mmoja,watatu wamejeruhiwa pamoja na polisi mmoja, " amesema Guillaume Djike.

Wanaharakati wa haki za binaadam wameelezea msimamo wao dhidi ya kukosekana kwa usalama jijini GOMA

“Ni viongozi ndio walio na jukumu la kuleta usalama kwa raai. Raia hawana uwezo wowote wa kudhibiti au kuleta usalama. Jeshi na polisi ndi wenye majukimu ya kusimamia usalama mahali pote nchini Congo, " amesema Placide Nzilamba, mmoja wa wanaharakati hao.

Kwa upande wao, wakazi wa mji wa Goma wamesema polisi ingewakamta waasi hao bila hata hivyo kuwaua ili wawasikilize madai yao. Lakini wengine wameelezea kuwa ukosefu wa usalama nchini DRC unasababishwa na mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini, hasa suala la uchaguzi.

Hivi karibuni wagonjwa zaidi ya 10 walijeruhiwa kwa visu katika hospitali jijini Goma baada ya hosptali hiyo kuvamiwa na kundi la wahalifu.