AFRIKA KUSINI-SIASA

Rais wa Afrika Kusini atangaza baraza jipya la mawaziri

Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa.
Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa. REUTERS/Rodger Bosch/Pool

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza baraza lake jipya la mawaziri, ambapo baadhi ya mawaziri wa zamani wameendelea kushikilia nafasi zao za zamani.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa zamani wa fedha Nhlanhla Nene aliyetimuliwa mnamo Disemba 2015 na rais wa zamani Jacob Zuma amerejeshwa tena katika nafasi hiyo. Nafasi ya Nene ilichukuliwa wakati huo na Des van Rooyen, lakini alihudumu kwenye nafasi hiyo katika kipindi kisichozidi siku nne. Na nafasi hiyo ikachukuliwa na Pravin Gordhan baada ya Randi kupoteza thamani.

Hatahivyo Rais Cyril Ramaphosa, amemteua Pravin Gordhan kuwa waziri wa masuala ya biashara.

Naye Nkosazana Dlamini-Zuma, mwenyekiti wa zamani wa tume ya Umoja wa Afrika, ameteuliwa kuwa waziri wa ofisi ya rais.

Katika baraza hilo jipya la Ramaphosa, watu wengine ambao ni wapya lakini wapiganaji wa zamani wa ANC walipewa wizara nyeti, hasa wale waliomsaidia kumtimua rais Jacob Zuma.

Aliingia madarkani baada ya mtangulizi wake kuondoka katika hali tete, baada ya kupinga shinikizo la chama chake la kujiuzulu.