BURKINA FASO-HAKI-USALAMA

Burkina Faso: Zaidi ya watu 80 wakabiliwa na mashitaka ya kupanga jaribio la mapinduzi

JeneraliGilbert Diendéré (kushoto) na waziri wa zamani wa mamabo ya nje wa Burkina Faso Djibrill Bassolé ni washukiwa wakuu katika kesi ya jaribio la mapinduzi ya mwezi Septemba 2015.
JeneraliGilbert Diendéré (kushoto) na waziri wa zamani wa mamabo ya nje wa Burkina Faso Djibrill Bassolé ni washukiwa wakuu katika kesi ya jaribio la mapinduzi ya mwezi Septemba 2015. Ahmed OUOBA / AFP

Zaidi ya watu 80 wamefunguliwa mashtaka katika Mahakama ya Kijeshi nchini Burkina Faso kwa jaribio la kuipindua serikali mwaka 2015.

Matangazo ya kibiashara

Kesi hiyo ambayo ilikua ilianza jana imesitishwa baada ya kuzuka utata kufuatia sheria inayomteua mkuu wa mahakama. Mawakili wa upande wa utetezi walitoka nje kabla ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa kwa undani.

Hii ni kesi ya kipekee katika taifa hilo la Afrika Magharibi na kipimo cha Haki dhidi ya washukiwa.

Miongoni mwa watu hao ni Majenerali wawili Gilbert Diendere na Djibrill Bassole wanaotuhumiwa kupanga jaribio la mapinduzi hayo.

Mahakama imeambiwa wawili hao waliwasili katika jiji kuu Ouagadougou na kupokelewa kwa shangwe na raia wa nchi hiyo.

Bassole na Diendere walikuwa washirika wa karibu sana wa rais wa zamani Blaise Compaore ambaye aliondolewa madarakani mwaka 2014.

Washukiwa hao wanatuhumiwa kwa makosa ya uhaini na kuhatarisha usalama wa taifa katika jaribio hilo lililosababisha vifo vya watu 14 na kusababisha majeruhi ya watu wnegine 270.

Kesi hii inaelezwa kuwa huenda ikachukua muda mrefu kabla ya hukumu kutolewa.