Wengi wajiuliza silaha zinazotumiwa na polisi kwa kukandamiza raia zinatoka wapi DRC

Vikosi vya usalama vya DRCkaribu na Kanisa la Notre Dame huko Kinshasa, Februari 25.
Vikosi vya usalama vya DRCkaribu na Kanisa la Notre Dame huko Kinshasa, Februari 25. REUTERS/Goran Tomasevic

Baada ya maandamano yaliyoitishwa na kanisa Katoliki kukabiliwa na ghasia zilizosababishwa na vikosi vya usalama nchini DRC, mashirika yasio ya kiserikali yameomba Umoja wa Ulaya na Ufaransa kutoa msimamo wao.

Matangazo ya kibiashara

Mashirika hayo yanajiuliza aina ya ushirikiano wao na vikosi vya usalama vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Je! Umoja wa Ulaya na Ufaransa wana uhusiano wa moja kwa moja au kupitia kampuni au kundi fulaani na ukandamizaji huu? Siku ya Jumatano Februari 28, Umoja wa Ulaya na Ufaransa walijibu. Umoja wa Ulaya ulisema unaendelea na mpango wa msaada kwa jeshi, lakini hasa katika usimamizi na utawala. Ubelgiji iko wazi kwa suala hilo. Imesema haitoi msaada wowote wa silaha. Ufaransa haitoi tena leseni za kusafirisha silaha tangu mwezi Novemba. Ushirikiano wa kijeshi ulibadilishwa kuwa wa mafunzo, na wala sio kwa opereshini za polisi au za kijeshi. Hakuna mfanyakazi au mtaalam kutoka Ufaransa ambaye ana uhusiano wowote na masuala ya usalama nchini DRC. Maswali mengi yameibuka na kujiuliza nani anayetoa silaha kwa vikosi vya usalama vya DRC kwa kukandamiza waandamanaji?

Katika miji mitatu ambapo kulishuhudiwa maandamano yaliyogubikwa na ghasia zilizosababishwa na ukandamizaji mkubwa wa vikosi vya usalama tangu Januari 2018, kasha za risasi zilizookotwa pembezoni au ndani ya makanisa ni risasi zilizotengenezwa nchini China zenye maandishi 7.62 x 39 mm za bunduki aina ya Kalashnikov.

Katika mji wa Mbandaka - ambapo mmoja wa waandamanajir, Eric Bokolo, aliuawa tarehe 25 Februari 2018 - kasha za risasi zilikua namba inayojulikana nchini DRC: 61/98. " 98" ni mwaka ambapo risasi hizo zilitengenezwa na "61" ni namba ya kiwanda kilichotengeneza risasi hizo, ambacho kimejulikana kuwa ni kiwanda cha China North Industries Corporation (Norinco).

Ikiwa risasi hizi za bunduki aina ya Kalashnikov zinajulikana na wataalamu wa silaha, ni kwamba zinapatikana katika makundi makuu ya waasi, mashariki mwa DRC tangu mwaka 2013. Bila shaka, kundi la zamani la waasi la M23, ambalo lilikua limeundwa kwa sehemu kubwa na maafisa waliotoroka jeshi la DRC, lakini pia kundi la waasi wa Kihutu wa Rwanda FDLR, kundi la waasi la Nyatura, APCLS na makundi mengine wanatumia risasi hizi.

Uswisi na kampuni ya Brüger & Thomet wanasema hawajawahi kutoa guruneti hizi (zilizookotwa baada ya ukandamizaji dhidi ya maandamano ya kanisa Katoliki) kwa polisi ya DR Congo.
Uswisi na kampuni ya Brüger & Thomet wanasema hawajawahi kutoa guruneti hizi (zilizookotwa baada ya ukandamizaji dhidi ya maandamano ya kanisa Katoliki) kwa polisi ya DR Congo. Sonia Rolley/RFI

Katika miji mbalimbali ambapo kulishuhudiwa ukandamizaji huo, risasi zilizotengenezwa na viwanda vya China ziligunduliwa.

Kwa hiyo ni dhahiri kusema kuwa huenda jeshi la DRC lina uhusiano na makundi mbalimbali ya waasi nchini humo kwa kupata silaha, risasi na vifaa vingine vya jeshi vinavyotumiwa kwa kukandamiza waandamaji.