Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-UGAIDI-UFARANSA

Kundi la kijihadi la GSIM ladai kushambulia ubalozi wa Ufaransa jijini Ouagadoudou

Madhara ndani ya gari dogo linaloaminiwa kubeba vilipuzi nje ya Ubalozi wa Ufaransa jijini  Ouagadougou.
Madhara ndani ya gari dogo linaloaminiwa kubeba vilipuzi nje ya Ubalozi wa Ufaransa jijini Ouagadougou. Ahmed OUOBA / AFP
Ujumbe kutoka: Victor Melkizedeck Abuso
1 Dakika

Kundi la kijihadi linaloshirikiana na kundi la al-Qaeda limedai kuhusika katika mashambulizi ya kigaidi katika Ubalozi wa Ufaransa na makao makuu ya jeshi jijini Ouagadoudou, nchini Burkina Faso wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi wanane waliuawa na wengine 12 kujeruhiwa katika makabiliano na wapiganaji wa kundi hilo la kijihadi linaloojiita GSIM.

Ripoti ya kundi hilo kupitia Shirika la Habari la Al-Akhbar nchini Mauritania, limesema lilitekeleza mashambulizi hayo kwa lengo la  kulipiza kisasi baada ya jeshi la Ufaransa kuwauwa viongozi wake Kaskazini mwa Mali wiki mbili zilizopita.

Taarifa za kijeshi kutoka Ufaransa zinasema, wanajihadi 20 waliuliwa katika makabiliano hayo.

Serikali ya Burkina Faso imesema inachunguza namna tukio hilo lilivyotokea ili kuwachukulia hatua waliohusika.

Ufaransa imesema, mashambulizi hayo yalilenga maslahi ya Ufaransa nchini Burkina Faso.

Paris imetuma kikosi chake cha wanajeshi 4,000 katika nchi za Sahel ambazo ni Burkina Faso, Niger, Mauritania, Chad na Mali kupambana na makundi ya kigaidi.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.