Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-UGAIDI-G 5 SAHEL

Viongozi wa ECOWAS walaani mashambulizi ya kigaidi nchini Burkina Faso

Marais kutoka ukanda wa Sahel barani Afrika , Roch Kaboré (Burkina), Idriss Déby (Tchad), Ibrahim Boubacar Keita (Mali), Mohamed Ould Abdel Aziz (Mauritanie), na  Mahamadou Issoufou (Niger)  walipokutana na rais wa Ufaransa mwezi Desemba mwaka 2017
Marais kutoka ukanda wa Sahel barani Afrika , Roch Kaboré (Burkina), Idriss Déby (Tchad), Ibrahim Boubacar Keita (Mali), Mohamed Ould Abdel Aziz (Mauritanie), na Mahamadou Issoufou (Niger) walipokutana na rais wa Ufaransa mwezi Desemba mwaka 2017 REUTERS/Ludovic Marin
Ujumbe kutoka: Victor Melkizedeck Abuso
1 Dakika

Marais wa Togo na Niger wamezuru jijini Ouagadougou nchini Burkina Faso kusimama na wananchi wa taifa hilo baada ya kundi la kijihadi kushambulia Ubalozi wa Ufaransa na Makao makuu ya jeshi iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo yaliyotekelezwa na kundi la GSIM, yalisababisha vifo vya wanajeshi nane na wengine kujeruhiwa.

Rais wa Togo Faure Gnassingbe ambaYe ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS, amesema mataifa hayo yataendelea kushirikiana kwa lengo la kushinda ugaidi Afrika Magharibi.

Naye rais wa Niger Mahamadou Issoufou ambaye ni rais wa nchi za Sahel zinazojumuisha, Burkina Faso, Niger, Mauritania, Chad na Mali, amesema vikosi vya nchi hizi vitaendelea kushirikiana na Ufaransa ili kushinda ugaidi.

Burkina Faso inasema inaendelea kuchunguza namna shambulizi hilo lilivyofanyika, wakati huu rais Roch Marc Christian Kabore akisema itachukua muda mrefu kushinda ugaidi nchini humo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.