AL SHABAB-SOKA-SOMALIA

Al Shabab yataka viwanja vya soka kufungwa Mogadishu

Mmoja wa uwanja wa soka katika mji wa Mogadishu nchini Somalia
Mmoja wa uwanja wa soka katika mji wa Mogadishu nchini Somalia AFP

Magaidi wa Al Shabab nchini Somalia wanataka kufungwa kwa viwanja vyote vya mchezo wa soka vinavyomilikiwa na watu binafsi katika wilaya tatu mjini Mogadishu.

Matangazo ya kibiashara

Radio Dalsan imeripoti kuwa tayari viwanja 20 vimefungwa katika wilaya za Karaan, Yaqshid na Heliwaa ili kutii agizo hilo la Al Shabab.

Ripoti zinasema kuwa hatua hii imekuja baada ya mkutano kati ya wamiliki wa viwanja hivyo na viongozi wa kundi la Al Shabab kufanyika hivi karibuni.

Al-Shabab haijasema sababu hasa ya kutaka viwanja hivyo kufungwa.

Inaelezwa kuwa kundi hilo ambalo liliondolewa Mogadishu mwaka 2011, limekuwa likitumia michuano ya soka katika maeneo mbalimbali kuwatafuta wapiganaji wapya.

Kundi hilo ambalo limesabibisha maelfu ya watu kupoteza maisha kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara.