DRC-UN-UCHAGUZI

UN yaridhishwa na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu nchini DRC

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres REUTERS/Tiksa Negeri

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema anaridhishwa na maandalizi yanayofanyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuelekea Uchaguzi Mkuu mwisho wa mwaka 2018.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, Guteress amesema anasikitishwa na namna polisi wanavyotumia nguvu dhidi ya waandamanaji wanaompinga rais Joseph Kabila wakimtaka ajiuzulu.

Hili limekuja wakati huu rais Joseph Kabila akikubali kukutana na Guteress ambaye atazuru nchi hiyo hivi karibuni.

Uchaguzi nchini DRC umepangwa kufanyika tarehe 23 mwezi Desemba, na Guteress amesema amefurahishwa na hatua ya serikali kuweka misingi ya kisheria kufanikisha Uchaguzi huo.

Hivi karibuni Tume ya Uchaguzi CENI, ilitangaza kuwa imepokea mitambo ya kieletroniki kuwatambua wapiga kura.

Rais Kabila ambaye amekuwa akiongoza nchi hiyo tangu mwaka 2001, hajasema ikiwa hawatania tena urais licha ya wasiwasi kuwa huenda akafanya hivyo kwa nguvu na kinyume cha sheria.