Pata taarifa kuu
DRC-MADINI-KABILA

Rais Kabila atia saini mswada wa madini kuwa sheria

Rais  Joseph Kabila, akihotubia wanahabari  mwezi Januari 2018 jijini Kinshasa
Rais Joseph Kabila, akihotubia wanahabari mwezi Januari 2018 jijini Kinshasa Thomas NICOLON / AFP
Ujumbe kutoka: Victor Melkizedeck Abuso
1 Dakika

Rais wa Jamhuri ya Kodemokrasia ya Congo Joseph Kabila ametia saini kuwa sheria mswada wa ongezeko la kodi kwenye madini hatua ambayo haikupokelewa vizuri na makampuni yanayofanya shughuli zao nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Mshauri wa rais Kabila ambaye hakutaka kutajwa, amethibitisha kiongozi huyo kutia saini mswada huo na kuongeza kuwa hakuna marekebisho yoyote aliyoagiza kufanyika na kwamba ameuridhia kama ambavyo bunge liliupitisha mwezi Januari.

Sheria hii mpya inachukua nafasi ya sheria ya mwaka 2002 kuhusu madini ambao Serikali ilidaiwa kuyapendelea makampuni ya kigeni.

Adha, inaruhusu utozwaji wa hadi asilimia 10 ya kodi kwenye madini muhimu nchini humo ikiwemo yale ya shaba na Colbat.

Hatua hii inakuja baada ya rais Kabila kukutana na wawekezaji wiki iliyopita kujadili sheria hii mpya na kuahidi kuwa matakwa yao yatasikilizwa baada ya kutiwa saini.

Wawekezaji wameonya kuwa huenda wakalazimika kuacha kuendelea kuwekeza au sheria hii ikawa kikwazo kwa wawekezaji wengine wanaotaka kuja kuwekeza katika sekta ya madini nchini DRC.

Wananchi wa DRC wanaendelea kuishi kwa umasikini mkubwa licha ya sehemu kubwa ya nchi hiyo kuwa na utajiri wa madini mbalimbali ikiwemo dhababu.

Uwepo wa madini haya umeendelea kuhatarisha usalama wa raia wa nchi hiyo kutokana na uwepo wa makundi ya waasi yanayowashambulia wanajeshi wa serikali na raia wa kawaida.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.