DRC-KATUMBI-UCHAGUZI

Katumbi kurejea nchini DRC mwezi Juni kujiandaa kuwania urais

Mwanasiasa wa upinzani nchini DRC  Moïse Katumbi, akiwa jijini Johannesburg Afrika Kusini alipokutana na wanasiasa wa upinzani Machi 11 2018
Mwanasiasa wa upinzani nchini DRC Moïse Katumbi, akiwa jijini Johannesburg Afrika Kusini alipokutana na wanasiasa wa upinzani Machi 11 2018 MUJAHID SAFODIEN / AFP

Kiongozi wa upinzani nchini DRC ambaye sasa anaishi uhamishoni Moise Katumbi Tschapwe, amesema atarejea nchini mwake mwezi Juni mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Gavana huyo wa zamani wa jimbo la Katanga, ametangaza pia atawania urais mwezi Desemba.

Akizungumza jijini Johannesburg ambako alikuwa amekutana na wanasiasa wa upinzani, Katumbi amesema watahakikisha wanapigana kuchukua madaraka.

Mwisho mwa wiki iliyopita, mamia ya wanasiasa wa upinzani walitangaza kumuunga mkono Katumbi kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka huu.

Mwansiasa huyo wa upinzani amesema lengo lake ya kutaka urais ni kuwasaidia wananchi wa taifa lake kuondokana na umasikini na kutatua changamoto za kiusalama.

Hata hivyo, ameendelea kutilia shaka, uwezo wa Tume ya Uchaguzi CENI kusimamia Uchaguzi utakaokuwa huru na haki.

Katumbi alikimbia nchi hiyo kwa sababu za kisiasa baada ya kukabiliwa na mashtaka kuhusu mikataba ya ardhi.

Mahakama imemhukumu kifungo cha miaka mitatu kutokana na mashtaka hayo ambayo amekuwa akisema yamechochewa kisiasa na rais Joseph Kabila.