MAURITIUS-UFISADI-SIASA

Rais wa Mauritius akataa kujiuzulu kwa madai ya ufisadi

Rais Mauritania Ameenah-Garib Fakim
Rais Mauritania Ameenah-Garib Fakim KAREL PRINSLOO / AFP

Rais wa Mauritius Ameenah Gurib-Fakim amekataa kujiuzulu licha ya tuhma za kutumia fedha za taasisi inayoshughulikia masuala ya Sayansi lenye mako yake jijini London nchini Uingereza Planet Earth Institute (PEI) kununua mavazi na vitu vingine vya kibinafsi.

Matangazo ya kibiashara

Gurib-Fakim, rais pekee mwanamke barani Afrika, ametuhumiwa kuchukua Dola 26,000 makusudi kutoka kwenye akaunti ya taasisi hiyo kwa matumizi binafsi.

Wiki iliyopita, Waziri Mkuu Pravind Jugnauth alitangaza kuwa rais huyo alikuwa amekubali kujiuzulu siku ya Jumatatu, siku ambayo nchi hiyo ilikuwa inaadhimisha miaka 50 ya uhuru wake.

Hata hivyo, rais huyo amesema madai hayo ni ya uongo na atahakikisha kuwa anasafisha jina lake, na hatajiuzulu.

“Mheshimiwa rais Ameenah Gurib-Fakim, hajafanya kosa lolote, hakuna ushahidi dhidi yake na hivyo anakataa shinikizo za kumtaka ajiuzulu,” taarifa kutoka Ikulu ilisomeka.

Hata hivyo, taarifa zinasema kuwa rais huyo alichukua fedha hizo kimakosa na tayari zimerejeshwa.