Pata taarifa kuu
SOMALIA-FARMAJO-WANAJESHI

Rais wa Somalia awafuta kazi Majenerali 18 wa kijeshi

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo REUTERS/Feisal Omar
Ujumbe kutoka: Victor Melkizedeck Abuso
Dakika 1

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo amewafuta kazi Majenerali 18 wa kijeshi nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema ni Majenerali wanne tu kati ya 22 katika jeshi la Somalia , ndio waliosalimika katika hatua hiyo ya kushangaza iliyochukuliwa na rais huyo.

Aidha, inaripotiwa kuwa hatua hii inalenga kusafisha jeshi la nchi hiyo katika mchakato wa kubadilisha mfumo wa usalama.

Rais Farmajo ameamua kwenda kufanya kazi akiwa ndani ya Wizara ya Ulinzi, kuongoza mabadiliko hayo.

Haya ni maamuzi yanayochukuliwa wakati huu serikali ya Somalia ikiendelea kukabiliana na ukosefu wa usalama kutokana na kuwepo kwa kundi la kigaidi la Al Shabab.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.