Pata taarifa kuu
NIGERIA

Nigeria: Wasichana wa shule waliotekwa waungana na familia zao

Wanafunzi wasichana waliotekwa kwenye shule ya mji wa Dapchi wakipokelewa na wazazi wao. 25 Machi 2018.
Wanafunzi wasichana waliotekwa kwenye shule ya mji wa Dapchi wakipokelewa na wazazi wao. 25 Machi 2018. RFIHAUSA/Bilyaminu Yusuf
Ujumbe kutoka: Emmanuel Richard Makundi
Dakika 2

Wasichana wa shule waliokuwa wametekwa na kundi la Boko Haram kwenye mji wa Dapchi kaskazini mwa nchi ya Nigeria, wameungana na familia zao baada ya majuma matano ya kuwa chini ya wapiganaji wa kundi hilo.

Matangazo ya kibiashara

Wasichana 105 waliokuwa wamefunika nyuso zao waliwasili wakiwa kwenye mabasi matano kwenye mji wa Dapchi jimboni Yobe ambapo walilakiwa na wazazi wao katika shule ya kulala ambako ndiko walikochukuliwa na wapiganani hao Februari 19.

Baada ya kuachiwa kwao Jumatano ya wiki iliyopita walitumia muda wa siku tatu mjini Abuja ambako walifanya mazungumzo na rais Muhammadu Buhari.

Kachalla Bukar baba wa mmoja wa wasichana waliotekwa na msemaji wa wazazi wengine amesema walisafirishwa kwa ndege kwenye kwenye mji wa Maiduguri kutokea Abuja na baadae kusafirishwa kwa mabasi ya jeshi kufika Dapchi.

“Furaha yangu haina mfani,” amesema Mai Gaji baada ya kuwapokea mtoto wake na mjukuu wake. “utekaji nyara hautanizuia kuwapeleka watoto wangu shule,” alisema.

Hata hivyo kwa Ali Gashomu ambaye mtoto wake alitekwa siku moja tu baada ya kumuandikisha shuleni tukio hili limemfanya aishi kwa hofu na hata kubaki na tashwishwi ikiwa atamrejesha tena shuleni mwanae.

Waziri wa habari Lai Mohammed amesema wasichana hao waliachiwa huru baada ya majadiliano na watekaji na kwamba hakuna kiasi chochote cha fedha kilicholipwa au kubadilishana wafungwa.

“Kile walichokitaka ni usitishaji mapigani ambayo yataruhusu watoto hao kurejeshwa,” alisema waziri aliyeongeza kuwa mapigani yalisitishwa kuanzia Machi 19.

Wasichana hao ni miongoni mwa wanafunzi 11 waliotekwa mwezi uliopita ambao watano kati yao walipoteza maisha wakati wa utekaji au wakiwa kwenye lori lililowapakakia.

Katika hatua nyingine watu 5 wameripitiwa kufa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulio la kundi la Boko Haram Kusini mwa nchi ya Niger jirani na mpaka wa nchi za Nigeria.

Shambulio hili linadaiwa kutekelezwa Ijumaa ya wiki iliyopita baada ya wapiganaji wake wenye silaha kushambulia watu kwenye soko moja katika mkoa wa Diffa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.