AFRIKA KUSINI-WINNIE MANDELA-JAMII

Winnie Mandela afariki dunia Afrika Kusini

Winnie Mandela, aliye kuwa mke wa Nelson Mandela Madiba, hapa ni Oktoba 30 mwaka 2014, akikataliwa kupewa umiliki wa makazi ya Qunu.
Winnie Mandela, aliye kuwa mke wa Nelson Mandela Madiba, hapa ni Oktoba 30 mwaka 2014, akikataliwa kupewa umiliki wa makazi ya Qunu. AFP PHOTO/GIANLUIGI GUERCIA

Mwanaharakati na mke wa zamani wa Rais wa kwanza mwafrika wa Afrika Kusini (hayati Nelson Mandela), Bi. Winnie Mandela amefariki leo Jumatatu mchana akiwa na umri wa miaka 81 jijini Johannesburg. Msaidizi wake, Zodwa Zwane amethibitisha taarifa hizo.

Matangazo ya kibiashara

Winnie Madikizela-Mandela (amezaliwa tarehe 26-09-1936 na jina la Nomzamo Winifred Zanyiwe Madikizela ) ni mwanasiasa wa Afrika Kusini, ambaye ameshikilia nafasi kadhaa serikalini na alikuwa mkuu wa vuguvugu la wanawake katika chama cha ANC.
Alikua bado mwanachama wa kamati ya kimataifa ya ANC.

Ingawa bado alikuwa mke wa Nelson Mandela wakati Mandela alipewa urais wa Afrika ya Kusini mnamo Mei 1994, kamwe hakuwa first lady wa Afrika ya Kusini, kwani wanandoa hawa walikuwa wametengana miaka miwili iliyopita.

Hii ilikuwa baada ya Winnie kugunduliwa kuwa na uhusiano wa kimapemzi na watu wengine baada ya kuachiliwa kwa Nelson kutoka gerezani mnamo Februari 1990.

Talaka ya mwisho ilipitishwa mnamo tarehe 19 Machi 1996.

Kama mwanaharakati mwenye utata, alikua maarufu miongoni mwa wafuasi wake ambao walimwita 'Mama wa Taifa'.
Lakini si wote waliompenda kwani wengine humtusi, hasa kutokana na madai kadhaa ya uhusika wake katika ukiukaji wa haki za binadamu, iliyohusisha mateso na mauaji ya mtoto wa umri wa miaka 14 aliyekuwa anaitwa Stompie Moeketsi mwaka wa 1989.

Nelson Mandela akiachiliwa huru baada ya kufungwa miaka 27.Hapa akiwa na mkewe Winnie Madikizela-Mandela, Februari 1, 1990.
Nelson Mandela akiachiliwa huru baada ya kufungwa miaka 27.Hapa akiwa na mkewe Winnie Madikizela-Mandela, Februari 1, 1990. Allan Tannenbaum