AFRIKA KUSINI-WINNIE MANDELA-JAMII

Afrika Kusini yaomboleza kifo cha Winnie Mandela

Afrika Kusini inaomboleza kifo cha mke wa zamani wa rais wa kwanza Mweusi wa nchi hiyo Nelson Madiba Mandela, aliyefariki jana Jumatatu Aprili 2, 2018.

Picha nyeusi na nyeupe ya Winnie Madikizela-Mandela iliyozungukwa na bendera za chama cha ANC, Durban Aprili 2, 2018.
Picha nyeusi na nyeupe ya Winnie Madikizela-Mandela iliyozungukwa na bendera za chama cha ANC, Durban Aprili 2, 2018. AFP
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Afrika Kusini imetangaza kwamba itaandaa matukio kadhaa kuhusu Winnie Mandela aliyejitoa muhanga kwa kupigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi.

Winnie Mandela alifariki jana Jumatatu katika hospitali ya Johannesburg akiwa na umri wa miaka 81 baada ya "ugonjwa wa muda mrefu", msemaji wake amesema. Winnie Madikizela Mandela, ambaye "alikuwa mojawapo ya wanaharakati wakubwa katika mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi", "alijitoa mhanga maisha yake kwa ajili ya uhuru wa Afrika Kusini," msemaji wake alisemasema.

Wafuasi wake ambao walikuwa wameanza kukusanyika mbele ya nyumba yake baada ya kutangazwa kifo chake siku ya Jumatatu, wameendelea kufurika mbele ya nyumba yake ya kifahari iliyojengwa kwa matofali yenye rangi nyekundu katika mji wa Soweto.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, kiongozi wa chama tawala cha African National Congress (ANC), pia alipigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi, amekaribisha ushujaa wa Winnie Madikizela Mandela katika harakati zake dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.

Rais Ramaphosa amesema, Afrika Kusini inaomboleza kifo chake na serikali itashirikiana na familia wakati wa mazishi yake rasmi Aprili 14 rasmi siku ya Aprili 14, alitangaza.

Siku ya Jumatatu usiku, Rais Ramaphosa alikwenda nyumbani kwa Winnie Mandela mjini Soweto, ambapo wafuasi wake walikua walikusanyika, wakiimba nyimbo za vita walizokua wakiimba wakati wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.