CAMEROON-USALAMA

Mateka 18 waachiliwa kusini magharibi mwa Cameroon

Idara za Usalama nchini Cameroon zimewaachia huru watu 18 waliotekwa nyara kusini-magharibi mwa nchi hiyo, miongni mwao raia saba kutoka Uswisi na Wataliano watano, msemaji wa serikali amesema.

Askari wa Cameroun wakipiga doria katika mji wa Bafut, kaskazini magharibi mwa Cameroon, katika eneo la watu wanaozungumza Kiingereza, mnamo Novemba 15, 2017.
Askari wa Cameroun wakipiga doria katika mji wa Bafut, kaskazini magharibi mwa Cameroon, katika eneo la watu wanaozungumza Kiingereza, mnamo Novemba 15, 2017. AFP
Matangazo ya kibiashara

Wengine sita ni wafanyakazi, raia wa Cameroon.

Mateka hao walitekwa nyara siku ya Jumatatu na kukombelewa na kikosi maalumu cha jeshi la Cameroon, amesema Issa Tchiroma Bakary, ambaye anashutumu "magaidi wanaotetea kujitenga" kuhusika na utekaji nyara huo.

Neno hili linatumiwa na serikali kwa kutaja wanaharakati kutoka maeneo yanayozungumza Kiingereza wanaotetea kujitenga kwa majimbo yao na kuitwa taifa huru la Ambazonia.

Vikosi vya ulinzi vya Ambazonia (ADF) vimefutilia mbali madai ya kuhusika kwao katika utekaji nyara huo.