SOMALIA-UGAIDI-AL SHABAB

Shambulizi la bomu laua watano uwanja wa soka nchini Somalia

Shambulizi la bomu katika uwanja wa soka Kusini mwa Somalia, limesababisha vifo vya watu watano.

Wapiganaji wa Al Shabab nchini Somalia
Wapiganaji wa Al Shabab nchini Somalia wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Hii ni mara ya kwanza kwa shambulizi la kigaidi kulenga uwanja wa michezo nchini humo.

Maafisa wanasema shambulizi hilo lilitokea katika mji wa Barawe jimboni Shabelle, wakati watu wakitazama mpira wa soka.

Polisi wanashuku kundi la kigaidi la Al Shabab kuhusika katika shambulizi hili ambalo limesababisha pia watu 12 kujeruhiwa.

“Tunaamini kuwa Al Shabab ndio waliohusika na ni bahati kuwa maafisa wa juu wa serikali hawakuwepo wakati mechi hiyo ikiendelea,” amesema Mohammed Aden.

Rais Abdullahi Mohamed amesema adui pekee wa nchi hiyo ni Al Shabab.