Pata taarifa kuu
DRC-UCHAGUZI-SIASA

CENI: Ni muhimu kutumia mashine za kupigia kura katika Uchaguzi mkuu DRC

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi DRC, Corneille Nangaa.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi DRC, Corneille Nangaa. Ceni Kinshasa

Tume ya Uchaguzi nchini DRC (CENI) imeendelea na msimamo wake wa kutumia mashine za kupigia kura katika uchaguzi ujao uliopangwa kufanyika Desemba 23. Hivi karibuni upinzani ulitishia kutoshiriki uchaguzi iwapo mashine hizo zitatumika kwa uchaguzi huo.

Matangazo ya kibiashara

Upinzani unaona kuwa ni hila za serikali kutaka kuiba kura, ukiistumu Tme ya Uchaguzi kufanya kazi kwa ushawishi wa serikali.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini humo, Corneille Nangaa amesema kuwa bila mashine hizo itakua vigumu uchaguzi kufanyika kwa tarehe iliopangwa ya Desemba 23.

Bw Nangaa amesema uchaguzi unaweza kufanyika hata kama upinzani utakua umesusia.

Wakati huo huo Naibu Mwenyekiti wa CENI, Norbert Basangezi ameonya kwa watu watakaopatikana wakijiandikisha zaidi ya mara moja kwa minajili ya kupata kadi ya kupiga kura, sheria itafuata mkondo wake.

"Mtu yeyote ambaye ataonekana amejirodhesha mara mbili au mara tatu katika vituo vyetu [ili kupata kadi ya kupiga kura] atafikishwa mbele ya mahakama," Naibu Mwenyekiti wa CENI, Norbert Basengezi, ameonya akiwa mjini Bukavu mapema wiki hii.

Uchaguzi nchini DRC umepangwa kufanyika Desemba 23 mwaka huu, lakini sitofahamu imeendelea kuhusu uchaguzi huo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.