Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA-HAKI

Monusco yagundua makaburi ya halaiki Djugu, Ituri

Nyapala, kijiji cha wilaya ya Irokpa, kilishambuliwa na sehemu nyingine kuchomwa moto mnamo mwezi Machi katika Mkoa wa Ituri, DRC. (Picha ya kumbukumbu).
Nyapala, kijiji cha wilaya ya Irokpa, kilishambuliwa na sehemu nyingine kuchomwa moto mnamo mwezi Machi katika Mkoa wa Ituri, DRC. (Picha ya kumbukumbu). RFI/Florence Morice

Katika ripoti iliyochapishwa Jumatano, Aprili 25, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC imesema kuwa imegundua makaburi ya halaiki katika jimbo la Djugu Urtu.

Matangazo ya kibiashara

Huu ni ujumbe wa kuchunguza mapigano kati ya jamii mbili hasimu Hema na Lendu, yaliyozuka Desemba 2017, na kusababisha vifo vya watu 263, ikiwa ni pamoja na wanawake 91, huku visa vya uporaji vikiripotiwa katika vijiji 120 na kuwepo kwa makaburi ya halaiki katika maeneo 5 ya Centre Blukwa na Maze Liba.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, wengi wa waathirika ni watu kutoka kundi la Tribal Hemisphere.

Wachunguzi walikuwa katika eneo la tukio tarehe 14 hadi 22 Machi, lakini ripoti yao bado imechelewa, kwani vurugu bado zinaendelea na hali ya wakazi wa vijiji hivyo kuyahama makazi yao inatatiza uchunguzi. Uchunguzi zaidi uko njiani kuanza, afisa mmoja wa polisi ambaye hakutaka kutaja jina lake amesema.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.