DRC-AFYA

Madaktari watakiwa kusitisha mgomo DRC

Kamati ya kitaifa inayotetea maslahi ya madaktari wa DRCongo (SYMECO) imetangaza kuwa mgomo uliokuwa umepangwa kufanyika Jumatatu hii Aprili 30 katika nchi nzima hautafanyika tena.

Kinshasa, DR Congo: Waangalizi wa polisi ya MONUSCO katika majadiliano na wafanyakazi wa hospitali ya Cinquantenaire wakati wa mgomo tarehe 15 Agosti 2016, Kinshasa.
Kinshasa, DR Congo: Waangalizi wa polisi ya MONUSCO katika majadiliano na wafanyakazi wa hospitali ya Cinquantenaire wakati wa mgomo tarehe 15 Agosti 2016, Kinshasa. Photo MONUSCO/John Bompengo
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Kamati hiyo Juvenal Muanda Nlenda, amesema serikali imekubali kujibu madai yao, ambayo ni ongezeko la mshara kwa asilimia 100 miongoni mwa madai mengine.

Madaktari nchini DR Congo walikua wanaomba serikali kuboresha mishahara yao, huku wakiishutumu kutoheshimu makubaliano walioafikiana mwaka jana kuhusu madai yao.

Madaktari waliku wanadai kupewa mshahara mzuri, malipo ya kazi zao za ziada, kutambuliwa kwa vyeo vyao na ufumbuzi kwa madaktari mia moja waliyofukuzwa kinyume cha sheria mwaka 2016 kwa mujibu wa madaktari hao, na ambao hufanya kazi tangu wakati huo bila malipo.

Jambo muhimu zaidi, madaktari walikua wanalalamikia ni makubaliano ya hivi karibuni yaliyosainiwa mnamo Septemba 2017 na yangelipaswa kutatua masuala yote hayo yanayozua utata. Kwa mujibu wa madaktari makubaliano hayo hayajawahi kutekelezwa.