CAR-USALAMA

Jamhuri ya Afrika ya kati yaomboleza vifo vya watu 24 waliouawa

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya kati Faustin Archange Touadera ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo vya watu wasiopungua ishirini na wanne waliouawa katika mapigano kati ya wapiganaji wenye silaha na vikosi vya serikali.

Rais wa Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadéra katika mkutano na waandishi wa habari tarehe 11 Aprili 2018 huko Bangui, baada ya mapigano katika wilaya ya PK5 kati ya Minusca, vikosi vya usalama vya ndani na makundi ya wanamgambo.
Rais wa Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadéra katika mkutano na waandishi wa habari tarehe 11 Aprili 2018 huko Bangui, baada ya mapigano katika wilaya ya PK5 kati ya Minusca, vikosi vya usalama vya ndani na makundi ya wanamgambo. FLORENT VERGNES / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mapigano hayo yalitokea katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangui ambapo kanisa Notre Dame lilishambuliwa pia.

Tume ya umoja wa Mataifa nchini humo MINUSCA imesema imeimarisha doria kwenye mji mkuu Bangui na hasa wilaya ya PK5 ambayo imekuwa kitovu cha vurugu za kidini na umiliki wa maeneo wa makundi ya wapiganaji.

Mapigano haya yanazusha maswali zaidi kuhusu uimara wa serikali ya nchi hiyo na uwepo wa vikosi vya MINUSCA.

Machafuko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati yamesababisha vifo vya watu wengi na maelfu wengine kulazimika kuyahama makazi yao.

Wadadisi wanasema kuwa vita hivyo vinachochewa kidini, lakini kuna mwingiliano wa kisiasa.