Pata taarifa kuu
SAHEL-USALAMA

Kikosi cha G5 Sahel kuanza operesheni zake hivi karibuni

Kwa mujibu wa wizara ya ulinzi ya Niger: "kikosi cha G5 Sahel kiko tayari kwenda uwanja wa mapambano ili kupambana na ugaidi."
Kwa mujibu wa wizara ya ulinzi ya Niger: "kikosi cha G5 Sahel kiko tayari kwenda uwanja wa mapambano ili kupambana na ugaidi." © RFI/Olivier Fourt
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Mawaziri wa Ulinzi wa nchi zinazochangia kikosi cha kikanda cha G5 Sahel wametangaza kwamba shughuli za kwanza za kikosi hicho zinatarajiwa kuwa hivi karibuni.

Matangazo ya kibiashara

Operesheni hizo zilizopangwa kufanyika mnamo mwezi Machi, hazijafanyika kutokana na ukosefu wa fedha kwa kikosi hicho na vibali kwa nchi zitakazotoa wanajeshi wao.

Mnamo mwezi Oktoba, operesheni ya kwanza iliyoitwa "Ng'ombe mweusi" ilipelekea Burkina Faso, Mali na Niger kuendesha operesheni ya kuyasaka makundi yenye silaha katika eneo la mipaka mitatu kati ya nchi tatu kwa msaada wa kikosi cha Ufaransa, Barkhane. Operesheni ambayo kila nchi iliendesha operesheni yake kwenye mipaka yake.

Bila ya kutoatarehe, Mawaziri wa ulinzi wa nchi wanachama wa G5 Sahel wametangaza kwamba operesheni ya kikosi cha G5 Sahel itaanza katika kupambana na makundi yanayohatarisha usalama katika mipaka ya nchi hizo. Wataalam katika masuala ya usalama wameanza kazi ya kuchunguza kama askari wote kutoka bataliani mbalimbali wana uwezo wa kupambana, ikiwa vifaa na maeneo ya kuingilia kati yanakidhi vigezo tofauti vinavyohitajika. Ni baada ya ukaguzi huu, ambapo shughuli zitazinduliwa kwa mujibu wa Moutari Kalla, Waziri wa Ulinzi wa Niger.

"Moja ya bataliani ya kikosi cha G5 Sahel tayari imethibitishwa na wataalam kama inafaa kutumwa katika uwanja wa mapigano," Bw. Kalla amesema. Askari wengine wako tayari na tumetoa wito kwa wataalam kwenda kujionea wenye hali halisi ya mambo, uwezo wa kikosi hicho ili kukubalisha na kuturuhusu kuwatuma kwa operesheni za baadaye. Kikosi cha G5 Sahel kiko tayari kwenda uwanja wa mapambano ili kupambana na ugaidi. "

Kikosi cha G5 Sahel kinajumuisha nchi tano: Burkina Faso, Mali, Niger, Mauritania na Chad, na kina askari 10,000.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.