AFRIKA KUSINI-DINI-USALAMA

Hali ya wasiwasi yazuka kwenye msikiti ulioshambuliwa Durban

Polisi kwenye lango wa msikiti ambapo watu wasiojulikana walishambulia waumini kwa visu, katika mji wa Durban, Mei 10, 2018. Imam aliuawa na watu wawili walijeruhiwa vibaya.
Polisi kwenye lango wa msikiti ambapo watu wasiojulikana walishambulia waumini kwa visu, katika mji wa Durban, Mei 10, 2018. Imam aliuawa na watu wawili walijeruhiwa vibaya. RAJESH JANTILAL / AFP

Nchini Afrika Kusini, polisi iligundua bomu siku ya Jumapili usiku, Mei 13, katika msikiti mmoja kaskazini mwa Durban. Msikiti huo ulivamiwa na watu wasiojulikana ambao walishambulia waumini kwa visu.

Matangazo ya kibiashara

Mtu mmoja aliuawa na wengine wawili walijeruhiwa. Hii ni mara ya pili ndani ya siku chache msikiti huu ukilengwa kwa mashambulizi. Polisi imefutilia mbali dhana ya shambulio la kigaidi.

Waumini wa Msikiti huo wanasema waliona kitu kama bomu kabla ya kuanza sala yao hapo jana na kuwaita maafisa wa Polisi ambao walithibitisha kuwa ni bomu.

Hali hii imezua wasiwasi nchini humo baada ya kubainika kuwa mahubiri ya itikadi kali yamekuwa yakifunzwa katika msikiti huo ulio katika mji wa Pwani wa Durban.

Ripoti zinasema kuwa, msikiti huo umefungwa kwa muda ili kuruhusu ucungunguzi wa tukio hilo.

Licha ya kifo cha mtu na wengine wawili kujeruhiwa baada ya kuvamiwa, hakuna yeyote aliyekamatwa.

Kiongozi mmoja wa dini hiyo ya Kiislamu amesema, msikiti huo ulilengwa kwa sababu ilikuwa inaegemea Waislamu wenye kutoka dhehebu la Shia.