GAMBIA-HRW-TRIAL-JAMMEH-HAKI

Rais wa zamani wa Gambia achunguzwa kwa madai ya mauaji ya wahamiaji

Yahya Jammeh mwenye vazi jeupe akiondoka mjini Banjul, kulia ni mlinzi wake akiwa analia. Januari 21, 2017
Yahya Jammeh mwenye vazi jeupe akiondoka mjini Banjul, kulia ni mlinzi wake akiwa analia. Januari 21, 2017 REUTERS/Thierry Gouegnon

Wahamiaji zaidi ya 50 kutoka Ghana na nchi nyingine za Magharibi mwa Afrika waliuawa kikatili na kikosi cha askari kiliokua chini ya udhibiti wa rais wa zamani wa Gambia Yahya Jammeh, kwa mujibu wa shirika la Kimataifa la Haki za Binadamu la Human Rights Watch na TRIAL International.

Matangazo ya kibiashara

Mauaji hayo yaliyotokea mnamo Julai 2005, yalitenga wahamiaji haramu - 44 kutoka Ghana na wengine wengi kutoka Nigeria, Senegal na Togo - ambao walikamatwa kwenye pwani ya Gambia wakati wakijaribu kufiingia Ulaya.

Walishukiwa kuwa askari mamluki waliokuja kuangusha utawala wa Yahya Jammeh, kwa mujibu wa taarifa ya Human Right Watch na TRIAL International, kupitia mahojiano yaliyofanywa miaka miwili iliyopita na maafisa 30 wa zamani wa usalama wa Gambia.

Ndani ya wiki moja, "Junglers", kikosi cha askari waliochaguliwa kutoka kikosi cha ulinzi wa taifa, kwa minajili ya ulinzi wa rais, "waliwaua kikatili wahamiaji nane karibu na mji mkuu Banjul na wengine kwenye mpaka wa Senegal, "mashirika haya mawili yamesema.

Ripoti ya pamoja ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika (ECOWAS) na Umoja wa Mataifa ambayo haikuwekwa hadharani, ilihitimisha wakati huo kwamba serikali haikuhusika "moja kwa moja wa la kutoa agizo lolote" katika mauaji yaliyotekelezwa " baadhi ya maafisa katika vyombo vya usalama wa Gambia, "walifanya hivyo kwa niaba yao wenyewe".

"Wahamiaji hawa kutoka Afrika Magharibi hawakuuawa na maafisa watovu wa nidhamu bali waliuawa na kundi la maafisa wa vikosi vya usalama kwa amri kutoka moja kwa mojakwa rais Jammeh," Reed Brody mwanasheria wa HRW amesema katika taarifa hiyo.

"Wasaidizi wa Jammeh kisha waliharibu ushahidi muhimu ili kuzuia wachunguzi wa kimataifa kujua ukweli," ameongeza.

Ufunguzi wa uchunguzi unaweza kupelekea serikali ya Ghanakuomba yahya Jammeh asafirishwe nchini humo, kwa mujibu wa mashirika hayo mawili

Yahya Jammeh, ambaye utawala wa miaka 22 uligubikwa na ukiukwaji wa haki za binadamu, alishindwa katika uchaguzi wa urais mnamo mwezi Desemba 2016 dhidi ya mgombea wa upinzani Adama Barrow.

Alilazimika kuondoka nchini mnamo mwezi Januari 2017 kwa na Kuelekea Equatorial Guinea baada ya majeshi ya ECOWASI kuingilia kati, kufuatia mgogoro mkubwa wa kisiasa, uliosababisha kukataa kuondoka madarakani.