DRC-EBOLA-WHO

DRC:Maambukizi ya Ebola yafika mji wa Mbandaka

Maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola yameripotiwa katika mji wa Mbandaka, wenye makaazi ya watu karibu Milioni moja umbali wa Kilomita 130 kutoka Kaskazini Magharibi mwa DRC ambako maambukizi ya kwanza yaliripotiwa mapema mwezi.

Watalaam wa afya wakiwa wamebeba mwili wa mtu aliyefariki baada ya kuambikizwa Ebola nchini DRC
Watalaam wa afya wakiwa wamebeba mwili wa mtu aliyefariki baada ya kuambikizwa Ebola nchini DRC appsforpcdaily.com
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imewapa wasiwasi watalaam wa afya kutoka DRC na Shirika la afya duniani WHO kuhusu namna ya kuudhibiti ugonjwa huu usisambae zaidi.

Waziri wa afya Oly Ilunga amethibitisha kutokea kwa maambukizi hayo katika mji huo ambao mtu mmoja amebainika kuambukizwa lakini haijafahamika iwapo alikutana na watu wengine.

Mji wa Mbandaka haupo mbali na jiji Kuu la Kinshasa, hali ambayo inazua wasiwasi kuwa huenda ukafika katika jiji hilo kuu.

Tangu kuzuka kwa ugonjwa huo katika eneo la Bikoro ambapo watu 23 wamepoteza maisha na wengine 42 kuambukizwa.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus siku ya Ijumaa anatarajiwa kutoa taarifa kamili kuhusu hali ya maambukizi ya ugonjwa huo nchini DRC.

Hii ni mara ya tisa kwa DRC kukumbukwa na Ebola, ugonjwa ambao uligunduliwa kwa mara ya kwanza nchini humo mwaka 1976.