DRC-EBOLA-WHO

Watu watatu zaidi waambukizwa Ebola mjini Mbandaka nchini DRC

Wizara ya afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza maambukizi mapya ya ugonjwa hatari wa Ebola katika mji wa Mbandaka.

Eneo lililoathiriwa na ugonjwa hatari wa Ebola Kaskazini Magharibi mwa DRC
Eneo lililoathiriwa na ugonjwa hatari wa Ebola Kaskazini Magharibi mwa DRC JOHN WESSELS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hii inafikisha idadi ya watu walioambukizwa kufikia 43 Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.

Hadi sasa watu 17 wamepoteza maisha katika janga hili la hivi punde.

Hata hivyo, Shirika la afya duniani WHO limesema maambukizi haya bado sio tishio la Kimataifa na jitihada zinafanyika kuudhibiti.

Katika taarifa yake WHO baada ya kukutana na mamlaka ya dharura ya afya imesisitiza kuwa hali ya mlipuko huo haijakidhi vigezo vya kutangazwa hali ya dharura nchini DRC.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa serikali ya Kidemokrasia ya Congo, WHO na washirika wamekuwa na mwitiko wa haraka na wa kina kufuatia hali hiyo.

Serikali ya Kinshasa ilitangaza kuzuka kwa virusi vya ebola katika jimbo la kaskazini magharibi Equateur mnamo Mei 8