Pata taarifa kuu
DRC-ADF-USALAMA

Watu 10 wauawa katika mashambulizi ya waasi wa ADF mashariki mwa DRC

Wilaya ya Beni, Kivu Kaskazini, DR Congo: Majeshi ya DRC FARDC na MONUSCO katika operesheni wakiyasaka makundi yenye silaha.
Wilaya ya Beni, Kivu Kaskazini, DR Congo: Majeshi ya DRC FARDC na MONUSCO katika operesheni wakiyasaka makundi yenye silaha. Photo MONUSCO/Force
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Watu kumi waliuawa usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu wiki hii na waasi wa Uganda wa Allied Democratic Forces (ADF) katika eneo la Beni, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa mujibu wa vyanzo vya habari.

Matangazo ya kibiashara

"ADF walishambulia mji wa Mbau (...), watu kumi walipigwa risasi na wengine wawili walijeruhiwa," alisema Jonas Kibwana, Mkuu wa wilaya ya Beni ambapo Mbau ni moja ya maeneo ya tarafa hiyo katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

"Wapiganaji wa ADF wlipenya na kuingia Magboko, waliiba katika maduka ya dawa na maduka mengine. Walipoona askari wetu wanakuja kuwashambulia, walianza kurusha risasi hivyo. Asubuhi hii tumeshuhudia vifo vya raia 10 na gari moja ambayo ilishimwa moto." Kapteni Mak Hazukay, msemaji wa jeshi katika eneo hilo ameliambia shirika la habari la AFP.

Mashambulizi yalitokea saa 12:30 jioni hadi usiku. Mashambulizi haya yanakuja wiki moja tu baada ya kufunguliwa kwa kesi nchini Uganda ya kiongozi wa ADF Jamil Mukulu.

Vyama vya kiraia vinashutumu jeshi (FARDC) kuchelewa kuingilia kati. "Tunalaani uzembe wa jeshi na idara za usalama katika nchi yetu. Wapiganaji wa ADF walifika saa 12:30 jioni, walitekeleza ukatili wao huo wakati ambapo jeshi lilikuwa chini ya mita 500" kutoka mahali pa shambulio hilo, "hatuelekatika wilaya ya Beni ameliambia shirika la habari la AFP.

Kundi la waasi la ADF linaendesha harakati zake mashariki mwa DRC kwa zaidi ya miaka 20 sasa, baada ya kutimuliwa nchini Uganda kwa kumpinga Rais wa nchi hiyo Yoweri Kaguta Museveni.

ADF wameshtumiwa na serikali ya DRC na Ujumbe wa Umoja wa Matiafa nchini humo (Monusco) kuua mamia kadhaa ya raia tangu mwaka 2014 katika eneo la Beni.

ADF pia wananashutumiwa kuua walinda amani watano kutoka Tanzania katika eneo la Beni manamo mwezi Desemba 2017.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.