Pata taarifa kuu
DRC-ADF-USALAMA

Waasi wasiopungua 10 wa ADF wauawa karibu na Beni, DRC

Majeshi ya DRC yameapa kulitokomeza kundi la waasi wa Uganda ADF.
Majeshi ya DRC yameapa kulitokomeza kundi la waasi wa Uganda ADF. REUTERS/Kenny Katombe
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Jeshi la DRC limetangaza kwamba limewaua waasi wasiopungua 10 wa kundi la waasi wa Uganda la Allied Democratic Forces (ADF) wakati wa operesheni iliyozinduliwa mapema asubuhi dhidi ya moja ya ngome yao wilayani Beni, mashariki mwa nchi hiyo..

Matangazo ya kibiashara

"Mapema mchana, tumekua na idadi ya waasi kumi wa ADF waliouawa katika mapigano kwenye barabara ya Mbau kuelekea Kamango," amesema Jenerali Marcel Mbangu, Mkuu wa operesheni dhidi ya waasi wa Uganda katika mkoa Kivu Kaskazini.

Tangu Asubuhi, milio ya risasi na milipuko ya mabomu imekua ikisikika katika eneo hilo la Beni, kwa mujibu wa mashahidi.

"Habari hii inatoa tumaini, jeshi limeanza kuonyesha ukakamavu wake, hata kama bado kuna wasiwasi kuhusu watu waliouawa," amesema Noella Muluwavyo, kiongozi wa shirika la kiraia katika wilaya ya Beni.

Usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu, ADF waliwaua raia kumi katika eneo hili, karibu mita 500 kutoka ngome ya jeshi, ambalo linashtumiwa na raia na mashirika ya kiraia kwamba ni "dhaifu".

ADF wanaendelea na vitendo vyao viouvu mashariki mwa DRC kwa zaidi ya miaka 20 tangu kukimbia baada ya kuanzisha vita dhidi ya rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni.

ADF wanashutumiwa na serikali ya DRC na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo (Monusco) kwamba wameua mamia kadhaa ya raia tangu mwaka 2014 katika wilaya ya Beni.

ADF pia wanashutumiwa kuhusika na mauaji ya walinda amani 15 kutoka Tanzania katika eneo hilo mnamo mwezi Desemba 2017.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.