DRC-ICC-BEMBA-HAKI

ICC yamuacha huru aliyekuwa makamo wa raisi DRC Jean-Pierre Bemba

Jean-Pierre Bemba, Hague, Jumatatu, Machi 21, 2016.
Jean-Pierre Bemba, Hague, Jumatatu, Machi 21, 2016. REUTERS/JERRY LAMPEN/Pool

Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC imemuachia huru aliyekuwa makamu wa rais wa DRC Jean-Pierre Bemba katika uamuzi wa rufaa aliyokuwa amekata kupinga hukumu ya miaka 18 jela kwa makosa ya uhalifu wa kivita.

Matangazo ya kibiashara

Bemba alipewa adhabu hiyo baada ya kupatikana na kosa la kuwaamuru wapigaji wake kwenda kutekeleza mauaji na makosa mengine ya ukiuwakji wa haki za binadamu katika nchi jirani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kwa mujibu wa mahakama hiyo Bemba hawezi kutiwa hatiani kwa makosa yaliyotekelezwa na majeshi yake nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati.

Mawakili wake waliomba majaji kupunguza adhabu hiyo, kwa sababu Bemba amekaa jela zaidi ya miaka 10.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa zamani (mwaka 200-2012) Adolphe Muzito amekumbusha kwamba Jean-Pierre Bemba hakuwa nchini Jamhuri ya Afrika kati ya mwaka 2002 na 2003 wakati uhalifu huo ulipofanyika.

"Jean-Pierre Bemba hakuwa moja kwa moja katika nchi hiyo kutekeleza uhalifu huo. Alipatikana tu na hatia kwa sababu alikua kiongozi tu na adhabu ambayo ametumikia ya miaka kumi jela inatosha. Wamuache aje ajiunge na wenzake kwa kulitumikia taifa lake, na kuongeza nguvu katika ukumbi wa siasa nchini kwa sababu bado ni maarufu, ana uzoefu mkubwa wa kisiasa . "

Hata hivyo viongozi wa mashtaka wanataka aongezewe kifungo jela ili kifikie miaka 25 kwa kile wanachosema, vitendo alivyofanya nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.