DRC-LUCHA-USALAMA-HAKI

LUCHA yataka uchunguzi kufanyika kuhusu kifo cha Nkulala

Nje ya mahakama ya Goma, wanaharakati vijana walikusanyika wakiwa na mabango ili kuwaunga mkono ndugu zao "Free Lucha," Februari 22, 2016.
Nje ya mahakama ya Goma, wanaharakati vijana walikusanyika wakiwa na mabango ili kuwaunga mkono ndugu zao "Free Lucha," Februari 22, 2016. © RFI/Sonia Roll

Vuguvugu la vijana wanaopigania Demokrasia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, LUCHA, wametaka kufanyika kwa uchunguzi wa kina kubaini mazingira ya moto yaliyounguza nyumba na kusababisha kifo cha mwanaharakati mwenzao Luc Nkulala.

Matangazo ya kibiashara

Vuguvugu hilo lenye makazi yake mjini Goma, limesema linahofia kuwa moto huo uliwashwa kwa makusudi na watu wanaopinga harakati zao za amani, na kwamba kifo cha Nkulala kina kila mazingira ya kutekelezwa kwa makusudi.

Vuguvugu la Lucha limekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha maandamano na migomo mashariki mwa nchi hiyo kushinikiza kuondoka madarakani kwa rais Joseph kabila ambaye amemaliza muda wake.

Baadhi ya wanaharakati wa vuguvugu hilo walikamatwa na kuwekwa jela kwa miezi kadhaa kabla ya kuachiliwa.

Uchaguzi nchini DRC umepangwa kufanyika mnamo mwezi Desemba, lakini LUCHA inataka uchaguzi huu kufanyika bila Kabila kuwa miongoni mwa wagombea urais.