MISRI-ETHIOPIA-USHIRIKIANO

Misri na Ethiopia zakubaliana kuondoa tofauti zao

Waziri Mkuu wa Ethipia Abiy Ahmed.
Waziri Mkuu wa Ethipia Abiy Ahmed. REUTERS/Tiksa Negeri

Wakuu wa nchi za Ethiopia na Misri wamekubaliana kuondoa tofauti zao na kujenga kuaminiana wakati wanapotatua changamoto zinazojitokeza na hasa kuhusu matumizi ya maji ya mto Nile, ambapo Ethiopia inajenga bwawa kubwa la kuzalisha umeme litakalotumia maji ya mto huo.

Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu Abiy Ahmed ambaye amefanya ziara ya siku mbili nchini Misri, amekutana na rais Abdel Fatta al-Sisi na viongozi hawa wawili kukubaliana kutengeneza uhusiano wa kimkakati ambao utajengwa katika ushirikiano na kuaminiana.

Mkurugenzi mkuu katika ofisi ya waziri mkuu wa Ethiopia, Fitsum Arega amesema viongozi hawa wawili pia wameelezea ahadi yao ya kuanzisha mfuko wa pamoja wa maendeleo ya miundombinu.

Wadadisi wanasema ziara hii ya waziri mkuu mpya wa Ethiopia itasaidia kupunguza sintofahamu baina ya nchi hizi mbili.