AFRIKA-AJIRA KWA WATOTO

Siku ya kimataifa ya kupinga ajira kwa watoto

Mamilioni ya watoto kati ya umri wa miaka 14 hadi 17 wameendelea kuajiriwa kwa sababu za umasikini hasa barani Afrika na kulazimika kuacha shule.
Mamilioni ya watoto kati ya umri wa miaka 14 hadi 17 wameendelea kuajiriwa kwa sababu za umasikini hasa barani Afrika na kulazimika kuacha shule. Alice Milot

Wakati dunia hivi leo ikiadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga ajira za watoto, Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya watoto milioni 152 duniani walio na umri wa kati ya miaka 5 hadi 17 wanatumikishwa duniani.

Matangazo ya kibiashara

Wataalamu wawili wa Umoja wa Mataifa kuhusu utumwa na kuuzwa kwa watoto wamesema kuwa zaidi ya watoto milioni 215 wanafanya kazi kote duniani huku zaidi ya nusu yao wakipitia hali ngumu zikiwemo dhuluma za kimapenzi na za kikazi.

Licha ya uwepo wa mikataba ya kimataifa na ya kitaifa kwenye nchi mbalimbali duniani, bado watoto wamekuwa wahanga kwa kutumikishwa kwenye kilimo, vita, migodini, biashara ya ngono na majumbani.

Mamilioni ya watoto kati ya umri wa miaka 14 hadi 17 wameendelea kuajiriwa kwa sababu za umasikini hasa barani Afrika na kulazimika kuacha shule.

Katika mataifa mengi ya Afrika, watoto huajiriwa kama wafanyakazi wa nyumbani, ambako wengi wao hukumbwa na dhuluma mbalimbali, zikiwemo dhuluma za ngono. Nimezungumza na Cynthia wairimu ambaye ni msichana wa umri wa miaka 17 na mabtye amefanya kazi za nyumbani kwa miaka mitatu sasa.