COTE D'IVOIRE-MAJANGA YA ASILI

Cote d'Ivoire: Watu zaidi ya kumi wafariki dunia Abidjan kufuatia mvua kubwa

Mji wa Abidjan unakabiliwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Mji wa Abidjan unakabiliwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. RFI/Frédéric Garat

Kulingana na ripoti ya GSPM, kikosi cha Zima Moto katika mji wa Abidjan, zaidi ya watu kumi wamefariki katika wilaya mbalimbali za mji mkuu wa kiuchumi wa Cote d'Ivoire. Watu zaidi ya sita wamefariki dunia katika wilaya ya Cocody Rieviera.

Matangazo ya kibiashara

Barabara karibu zote zimeharibika. Maafisa wa Zima Moto wametumwa katika mji huo tangu usiku wa kuamkia Jumanne wiki hii. Watu zaidi ya kumi na tano wamepoteza maisha, kwa mujibu wa mashahidi.

Mvua hizo zimesababisha maporomoko ya udongo na uharibifu mkubwa katika nyanja mbalimbali.

Kutokana na hali hiyo, serikali ya Cote d'Ivoire imetangaza mradi wa usafi wa mazingira utakaogharimu Faranga za CFA bilioni 530katika kipindi cha mwaka 2018-2033 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu.