COTE D'IVOIRE-MAJANGA YA ASILI

Serikali ya Cote d'Ivoire yatoa msaada kwa waathirika wa mafuriko

Ziara ya Rais Alassane Ouatarra kwenye eneo la mafuriko huko Abidjan.
Ziara ya Rais Alassane Ouatarra kwenye eneo la mafuriko huko Abidjan. Photo: Frédéric Garat / RFI

Baada ya mafuriko yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 15 huko Abidjan mwanzoni mwa wiki hii, serikali imetangaza kutoa Faranga za CFA bilioni mbili (sawa na Euro milioni tatu) kwa familia za waathirika na watu waliopoteza mali zao katika tukio hilo.

Matangazo ya kibiashara

Msaada wa chakula na mahitaji ya msingi pia vitatolewa. Na, baada ya kikao cha dharura cha Baraza la Usalama, Rais Alassane Ouattara alizuru eneo la tukio.

Rais Alassane Ouattara alijionea mwenyewe kwa macho yake jinsi hali ilivyokua katika mji wa Allabra, mji ambao umeathirika zaidi na mafuriko yaliyoikumba baadhi ya maeneo ya nchi hiyo mwanzoni mwa wiki hii. "Tumechukua uamuzi, tutasaidia kwa kweli." Baadhi ya familia zilimuelezea rais Outtara mazingira ambamo wanaishi huku baadji wakisema kuwa maji yamekua yakiongezeka kwa kiasi kikubwa ndani ya nyumba zao.

"Tutaleta msaada wetu wa kutosha. Tutawapa watu sehemu za kujihifadhi kuhakikisha usalama wao. Tutakuwa na mfumo wa tahadhari ikiwa mvua nyingine zitatokea. Tunaandaa mfululizo mzima wa utaratibu kama inavyotakiwa kuwa kwa nchi zilizoendelea. Naweza kuwaambia kwamba tutaendelea, " amesema rais wa Cote d' Ivoire.

Mwanzoni mwa wiki hii zaidi ya watu kumi walifariki katika wilaya mbalimbali za mji mkuu wa kiuchumi wa Cote d'Ivoire. Watu zaidi ya sita walifariki dunia katika wilaya ya Cocody Rieviera.

Kutokana na hali hiyo, serikali ya Cote d'Ivoire ilitangaza mradi wa usafi wa mazingira utakaogharimu Faranga za CFA bilioni 530katika kipindi cha mwaka 2018-2033 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu.