Pata taarifa kuu
GUINEA-AJALI

Wanne wafariki dunia katika ajali ya ndege ndogo nchini Guinea

Mfano wa ndege aina ya Let 410 iliyotengenezwa nchini Jamhuri ya Czech tarehe 7 Desemba 1999.
Mfano wa ndege aina ya Let 410 iliyotengenezwa nchini Jamhuri ya Czech tarehe 7 Desemba 1999. AFP
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Watu wanne walifariki dunia Jumapili, mwishoni mwa juma hili katika ajali ya ndege ndogo nchini Guinea, kwa mujibu wa vyanzo vya Wizara ya Ulinzi na na mamlaka ya uwanja wa ndege nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Ndege hiyo iliyokua imekodiwa na kampuni ya madini ya Dinguiraye (SMD), ilianguka karibu na Souguéta, mji mdogo katikati mwnchi, watu wanne waliokuwa ndani ya ndege hiyo walifariki pao hapo, Wizara ya Ulinzi ya ulinzi imesema.

Waathirika hao walikuwa raia wa Guinea, Ujerumani, Poland na Cape Verde, chanzo kutoka mamlaka ya uwanja wa ndege ambacho hakikutaja jina kililiambia shirika la habari la AFP.

Ndege hiyo yenye chapa 410 iliyoyengenezwa nchini Jamhuri ya Czech, ilikua ikimilikiwa na shirika la ndege la Aigle Air, kwa mujibu wa chanzo hicho.

"Watu waliokua katika ndege hiyo wote, waliangamaia katika ajali hiyo," ambapo sababu za ajali hiyo "bado hazijajulikana," amesema msemaji wa Wizara ya Ulinzi, Aladji Cellou Kamara.

"Tume ya uchunguzi imeundwa na inajumuisha watu kutoka Wizara ya Usafiri, Mamlaka ya uwanja wa ndegel, ili kujaribu kujua sababu, mazingira na jukumu la kila mmoja kuhusiana na ajali hiyo," Bw Kamara ameongeza.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.