DRC-KATUMBI-HAKI

Kesi ya Moise Katumbi yasikilizwa DRC

Kesi ya mwanasiasa wa upinzani DRC, Moise Katumbi, ambaye yuko uhamishoni, imesikilizwa Jumatano huko Kinshasa.
Kesi ya mwanasiasa wa upinzani DRC, Moise Katumbi, ambaye yuko uhamishoni, imesikilizwa Jumatano huko Kinshasa. Getty Images

Kesi inayohusu askari mamluki ambapo anahusishwa Moise Katumbi Chapwe, gavana wa zamani wa Katanga imesikilizwa leo Jumatano mbele ya Mahakama Kuu mjini Kinshasa, mji mkuu wa DRC.

Matangazo ya kibiashara

Mamia ya wafuasi na wapenzi wa mwanasiasa huyo wa upinzani wamehudhuria kesi hiyo.

Gavana wa zamani wa Katanga anashutumiwa "kuhatarisha usalama wa taifa DRC".

"Moise Katumbi Chapwe ambaye alitangaza kuwania katika kinyang'anyiro cha urais manmo Desemba 23, 2018 anashutumiwa kuajiri askari mamluki kwa lengo la kuhatarisha usalama wa nchi.

Moise Katumbi ambaye yuko uhamishoni anashtumiwa katika kesi hiyo pamoja na watu wengine watano, ikiwa ni pamoja na raia mmoja kutoka Marekani.