Pata taarifa kuu
SENEGAL-HAKI

Kesi ya aliyekuwa meya wa Dakar yaanza kusikilizwa

Khalifa Sall akiwasabahi wafuasi wake alipoondoka mahakamani tarehe 23 Januari 2018.
Khalifa Sall akiwasabahi wafuasi wake alipoondoka mahakamani tarehe 23 Januari 2018. RFI

Kesi ya Rufaa inayomkabili aliyekuwa meya wa zamani wa jiji la Dakar nchini Senegal, Khalifa Sall itaanza kusikilizwa Jumatatu wiki hii baada ya kusimamishwa kwa muda wa mwezi mmoja kuruhusu upande wa utetezi kujiandaa.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya kwanza, Ilimhukumu meya huyo wa Dakar kifungo cha miaka 5 jela kufwatia kosa la Ubadhirifu na ufujaji wa fedha za serikali.

Khalifa Sall amkuwa akiitaja kesi hiyo kuwa ni ya kisiasa.

Nayo Jumuia ya ECOWASS ilitupilia mbali hukumu ya mahakama ya mwanzo ikisema kuwa haikuwa ya haki.

Wakili Démba Ciré Bathily, mmoja wa watetezi wake Khalifa Sall, amesema muda umefika kwa mteja wake kuachiliwa huru.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.