TUNISIA-USALAMA

Polisi sita wauawa katika shambulizi Tunisia

Maafisa sita wa vikosi vya usalama wameuawa katika shambulizi la bomu kaskazini magharibi mwa Tunisia, shambulizi lililodaiwa kutekelezwa na kundi la Aqmi lenye mafungamano na Al Qaeda.

Mwili wa mmoja kati ya maafisa wa vikosi vya usalama vya Tunisia waliouawa kaskazini magharibi mwa Tunisia, katika hospitali ya Charles Nicole huko Tunis, Julai 8, 2018.
Mwili wa mmoja kati ya maafisa wa vikosi vya usalama vya Tunisia waliouawa kaskazini magharibi mwa Tunisia, katika hospitali ya Charles Nicole huko Tunis, Julai 8, 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Mazishi ya polisi hao yamefanyika Jumatatu wiki hii asubuhi skaribu na mji wa Tunis.

Mashambulizi hayo, ambayo yamesababisha vifo vingi tangu miaka miwili iliyopita, wakati ambapo Tunisia, inayokabiliwa na mgogoro wa kisiasa, ina matumaini mazuri mwaka huu kwa kuwapokea watalii wengi baa ya kuboresha hali usalama.

Mafisa sita wa kikosi cha ulinzi wa Taifa waliuawa na watatu walijeruhiwa wakati gari lao lilishambuliwa siku ya Jumapili asubuhi na bomu lililotengenezwa kienyeji karibu na mpaka na Algeria katika eneo la Ain Sultan (mkoa wa Jendouba, Wizara ya Mambo ya Ndani imesema.

Msemaji wa wizara hiyo, Jenerali Sofiene al-Zaq, ameelezea shambulio hilo kama la "kigaidi".

Aliongeza kuwa washambuliaji "walifyatulia risasi vikosi vya usalama" baada ya mlipuko, na kwamba "operesheni ya kuwasaka magaidi" inaendelea kwa ushirikiano na jeshi.

Usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu wiki hii, kundi la Aqmi, Okba ibn Nafaa, lenye mafungamano na Al Qaeda, lilidai kuwa kuwa lilitekeleza shambulio hili, huku likidai kwamba lilikamata silaha kadhaa kutoka kwa kikosi hicho kilicholengwa.