EQUATORIAL GUINEA-SIASA

Upinzani walalama kuhusu msamaha wa rais kwa wafungwa Equatorial Guinea

quatorial Guinea licha ya rais Teodoro Obiang Nguema kutoa mshama kwa wafungwa wote wa kisiasa Julai 4, kiongozi wa upinzani nchini Malabo ameliambia shirika la habari la AFP.

Rais wa Equatorial Guinea Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, anataka kuona kunafanyika mjadala wa kitaifa utakaojumuisha pia wanasiasa, mjadala ambao sasa umepangwa kufanyika mwezi Julai.
Rais wa Equatorial Guinea Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, anataka kuona kunafanyika mjadala wa kitaifa utakaojumuisha pia wanasiasa, mjadala ambao sasa umepangwa kufanyika mwezi Julai. REUTERS/Amr Abdallah Dalsh
Matangazo ya kibiashara

"Sheria haijatekelezwa nchini Guinea ya Equatorial, serikali haiiheshimu: rais ameamua kutoa msamaha wa jumla kwa wafungwa wa kisiasa tangu Julai 4, lakini watu bado wanazuiliwa jela," amesema Gabriel Nse Obiang, kiongozi wa chama cha CI, kilichofutwa tangu mwezi Februari mwaka huu.

Wafuasi thelathini wa chama cha IC wanazuliwa jela huko Evinayong (katikati mwa nchi) na wanasubiri kuachiliwa.

"Tunaomba maelezo zaidi kutoka serikali," amesema Obiang. "Ikiwa mfungwa mwingine wa kisiasa atafariki dunia katika jela wakati angelikua ameachiliwa huru, ni nani atakayewajibika?"

Bw Obinag anasema, tangu msamaha huo kutolewa na rais karibu wiki moja iliyopita, "bado ni marufuku kwa wafungwa wa chama cha CI kutembelewa na watu kutoka familia zao, sheria inakanyagwa na wale ambao wangelipaswa kuiheshimisha".

Hatua hiyo ilichukuliwa na rais Teodoro Obiang Nguema kabla ya "majadiliano ya kitaifa" ambayo mwenyewe aliitisha kuanzia Julai 16 hadi 21, "kuruhusu ushiriki mkubwa wa wadau wote wa kisiasa" katika mkutano huu.

Msamaha ulikuwa mojawapo ya masharti makuu yaliyowekwa na upinzani wa ndani na wananchi waishio nchi za kigeni kushiriki katika majadiliano ya kitaifa.