Pata taarifa kuu
UFARANSA-SENEGAL-HAKI

Mahakama ya Monaco yakataa kuzuia mali ya Karim Wade

Karim Wade, mtoto wa rais wa zamani wa Senegal, aliyetuhumiwa kujitajirisha kinyume cha sheria.
Karim Wade, mtoto wa rais wa zamani wa Senegal, aliyetuhumiwa kujitajirisha kinyume cha sheria. AFP PHOTO / STRINGER

Mahakama ya Monaco, nchini Ufaransa, imefutilia mbali ombi la serikali ya Senegal la kuzuia fedha za Karim Wade zilizowekwa kwenye benki za Monaco.

Matangazo ya kibiashara

Karim Wade, mtoto wa rais wa zamani wa Senegal Abdoulaye Wade, na mpinzani wa serikali alihukumiwa nchi Senedal kwa kosa la "kujitajirisha kinyume cha sheria".

Katika uamuzi uliotolewa Jumanne na kufichuliwa Jumatano wiki hii gazeti la Monaco-Matin, majaji wa Mahakama ya Jinai ya Monaco walikataa ombi la Senegal, ambayo ilitaka mahakama hasa kuzuia dola 2,000,000 za Karim Wade.

Karim Wade, mtoto na waziri wa rais wa zamani Abdoulaye Wade (2000-2012), alihukumiwa mwaka 2015 nchini Senegal hadi miaka sita jela, kutakiwa kulipa faini ya zaidi ya euro milioni 210 kwa kosa la "kujitajirisha kinyume cha sheria" na mali yake yote kuzuiwa.

Uamuzi huo ulithibitishwa na Mahakama Kuu, lakini alipata msamaha wa rais mwezi Juni 2016 na tangu hapo anaendelea kuishi uhamishoni.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.