DRC-USALAMA-SIASA

Joseph Kabila afanya mabadiliko katika jeshi la DRC

Rias wa DRC Joseph Kabila katika mkutano na waandishi wa habari Januari 26, 2018.
Rias wa DRC Joseph Kabila katika mkutano na waandishi wa habari Januari 26, 2018. Thomas NICOLON / AFP

Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo joseph Kabila amefanya mabadiliko katika jeshi la serikali ya nchi hiyo, FARDC ambapo baadhi ya maafisa waliokuwa kwenye usimamizi wa jeshi la Polisi nchini humo wamepewa nyadhifa muhimu ndani ya jeshi la nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa maafisa hao ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la polisi John Numbi Banza Tambo ambaye amekuwa akituhumiwa kuhusika na mauaji ya mwanaharakati Floribert Chebeya aliyeuawa akiwa mikononi mwa Polisi Juni 02 mwaka 2010, jijini Kinshasa.

Haya yanajiri wakati ambapo mvutano wa kisiasa nchini DRC unaendelea kutokota, huku wanasiasa wakitaka matumizi ya mashine za kielektroniki za kupigia kura wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Desemba 23 mwaka huu.

Baadhi ya wanasiasa hasa wale wa upinzani wanasema hawatoshiriki uchaguzi iwapo Joseph Kabila atawania kwenye kiti cha urais katika uchaguzi huo.