EQUATORIAL GUINEA-SIASA

Mazungumzo ya kisiasa bila vyama vikuu vya upinzani yaanza Equatorial Guinea

Rais wa Equatorial Guinea Teodoro Obiang Nguema Mbasogo.
Rais wa Equatorial Guinea Teodoro Obiang Nguema Mbasogo. REUTERS/Amr Abdallah Dalsh

'Mazungumzo ya kitaifa' yanayotakiwa na Rais Teodoro Obiang Nguema yameanza Jumatatu wiki hii nchini Equatorial Guinea. Hata hivyo viongozi wa vyama vikuu vya upinzani wahakushiriki mazungumzo hayo.

Matangazo ya kibiashara

Hatua kuhusu wafungwa wa kisiasa ambao walitakiwa kuachiliwa huru baada ya rais kutangaza kuwa ametoa msamaha kwa wafungwa hao, bado haijatekelezwa.

Rais Obiang, madarakani tangu mwaka 1979, awali alisema lengo lake ilikua "kuwezesha kushiriki kwa idadi kubwa ya wadau wote wa kisiasa" ili "kutunza amani na maendeleo ambavyo nchi inahitaji wakati huu."

Aliahidi kutoa "uhuru" na "usalama" kwa washiriki wote katika mazungumzo hayo, ambayo yangelijumuisha, kwa mara ya kwanza, mashirika ya kiraia, viongozi wa dini hasa kanisa Katoliki na jumuiya ya kimataifa.

Lakini Jumatatu wiki hii, hakuna uamuzi wowote uliotekelezwa kuhusu kuaachilia huru wafuasi wa chama kikuu cha upinzani cha CI wanaozuiliwa ambao wangelikua wameachiliwa huru, baada ya tangazo la rais la kutoa msamaha kwa wafungwa wa siasa, mapema mwezi huu.

"Kutokana na hali hii ya kisiasa, hatutarajii kitu chochote kutoka kwa mzungumzo haya," Gabriel Nse Obiang, kiongozi wa CI, amesema Jumatatu.

Chama cha CI kilifutwa mnamo mwezi Februari na wafuasi wake 30 wamefungwa gerezani tangu mwishoni mwa mwaka 2017. Chama, ambacho hakijaalikwa katika mazungumzo jhayo, tayari kimesema mazungumzo hayo "yameshindwa".

Vyama kumi na saba vilivyosajiliwa kisheria nchini humo vimethibitisha kuwa vinashiriki mazungumzo hayo.